SHAIRI - NI SHIBE AU MIMBA!
NI SHIBE AU MIMBA
Ni shairi ambalo linakemea
Vitendo viovu vinavyofanywa
Na mabinti wanaotoa mimba
Linaelezea kitu kinachopaswa
Kutolewa tumboni ni SHIBE
Na wala sio MIMBA, karibu!
Watunzi : Ziggy na
Muhsin
ZIGGY:
Hawana hata aibu,
Mila zetu kuharibu,
Ni kipi kimewasibu,
Ni shibe au mimba!
MUHSIN:
Wameikosa adabu,
Wakufuru kwa mababu
Ni ipi yao sababu,
Ni shibe au mimba!
ZIGGY:
Bado ninakosa jibu,
Ni laana za mababu,
Ya nini tupate tabu,
Ni shibe au mimba!
MUHSIN:
Dunia ina ajabu,
Utandawazi sababu,
Wasichana mna tabu ,
Ni shibe au mimba!
ZIGGY:
Hebu tupeni sababu,
Mtoto kumuharibu,
Mtapatwa na adhabu,
Ni shibe au mimba!
MUHSIN:
Hio nayo ndo sababu,
Ng’ombe aota sharubu,
Kwa yenu maajabu,
Ni shibe au mimba!
ZIGGY:
Hata na wavaa ijabu,
Mungu mwampa ghadhabu,
Na kihama ki karibu,
Ni shibe au mimba!
MUHSIN:
Mwaitafuta adhabu,
Mwendako iwaadhibu,
Watoto kuwa haribu,
Ni shibe au mimba!
ZIGGY:
Mimba uipate klabu,
Mmeshakunywa urabu,
Dhambi zenu mzitubu,
Ni shibe au mimba!
MUHSIN:
Mbona mwaiga ububu,
Huku mwashika sharubu,
Beti zataka mtubu,
NI SHIBE WALA SI MIMBA!


Comments
Post a Comment