NAKUCHUKIA CHIMWAGA - SEHEMU YA KWANZA
NAKUCHUKIA CHIMWAGA
Ukiachana na
siafu, sisimizi ndio wadudu wadogo ambao hukusanyika kwa pamoja kuongozana
kwenye shughuli zao za kila siku, mfano kwenye mambo ya ujenzi na hata kupeana
sapoti kwenye maswala ya mnuso, hakika huu msululu umeshona, kushoto na kulia
ni kundi kubwa la wanafunzi wakielekea CHIMWAGA zikisikika sauti tofauti za
wanachuo wa course mbalimbali kwa kuwa somo la leo wanasoma wanafunzi wa
faculty zote kwa mwaka wa kwanza wa masomo.
Nilistushwa na
mkono mlaini ulonigusa begani ukanifanya nipunguze speed ya hatua zangu na
kuvua earphone, “Msimbe!!!, kukuita kote huko hujanisikia!?” nikiwa namalizia
kutoa earphone ya sikio la pili akaongezea “mwanzoni nilijua nakufananisha, za
masiku!?” nikamjibu “safi tu” japo kuwa sura yake bado ilikuwa ngeni machoni
pangu. “Sorry, nikumbushe walau jina kama hautojali” akatahamaki “hakika
nimekufananisha, duniani wawili wawili kwa kuwa Msimbe sio wa kunisahau mimi”
Nikiwa bado nimemkazia macho, niligundua hakika
alikuwa ni binti mrembo mwenye kila sifa za uzuri ambao si rahisi kukutana na
aina ya watu hao mara kwa mara, nilianza kujiona mwenye bahati kusimama na
msichana mwenye sifa za kipekee mbele ya umati wa wanachuo, nilitamani kuwa
Msimbe kweli, ili niendelee kuongozana na binti huyo ambaye alionekana kuishiwa
nguvu ya maongezi baada ya kunifananisha.
“Pole, naitwa Justine. Ni mwaka wa kwanza, natokea
mkoa wa Morogoro, ni kweli utakuwa umenifananisha, kwani una uhusiano gani na
Msimbe! Mmepotezana muda sana!?” nilimuacha ajielezee, tukiwa bado tunaongozana
“Ahsante, alikuwa rafiki yangu nilisoma nae shule ya msingi miaka saba
iliyopita” alijibu huku akipepesa macho chini, mfano wa mwizi aliyeshikwa na
ushahidi wa mali ya dhuluma mkononi mwake.
“Usijali, naweza kulijua jina lako tafadhali!?”,
“naitwa Grace pia ni mwaka wa kwanza” nilitamani kubadilisha mada ili
tuendeleze conversation lakini tulikuwa tayari tumeingia malango ya Chimwaga,
na kwa uchache wa haya maongezi tuliyoongea hayakutosha kuwa na ujasiri wa
kuchukua hata namba zake za simu. Aligeuka nyuma na kuungana na jopo la
marafiki zake na kuniaga, “sawa Justine, wacha niwasubiri wenzangu niingie nao”
nami bila hiana “Usijali Grace, mimi natangulia ndani, ulisema unachukua course
gani?” nilimuuliza kwa kupata urahisi wa kumtafuta siku nyingine. “BADS”
alifupisha akimaanisha Bach of Arts in Development Study, tukaachana.
Niliingia darasani nikiwa bado natafakari uumbaji wa
Mungu, nilijinong’oneza mwenyewe kwa kujiambia ‘Mungu ni fundi’ nikiwa darasani
sikuelewa somo lolote kutoka kwa Lecture mawazo yote niliyaelekeza kwa Grace,
nilitamani kipindi kiishe mapema nimtafute John ambaye ni roomate wangu ambaye
pia anachukua BADS ili nimuelezee juu ya habari ya siku nzima ya leo iliyozidi
kunichanganya, upole na ukauzu wangu nikiwa chuo ulinifanye niwe mnyonge kila
utakaponiona sababu kwangu ilikuwa ni kazi kuchangamana na marafiki wapya, huwa
inachukua muda mrefu sana kuwazoea, pindi lilivyoisha kama kawaida nilivaa
earphone zangu na kurejea hostel.
Licha ya kuweka sauti ya juu ya muziki kwenye simu,
sikusikiliza neno lolote lililotajwa kwenye nyimbo, nikiendelea kupepesa macho
kwa kudhani nitaonana tena na yule binti mrembo lakini kwa wingi wa watu
waliotoka CHIMWAGA haikuwa rahisi kumtambua, niliongeza hatua kukazana kurudi
hostel nimuwahi John. Nilipofika room sikukutana na roomate yoyote niliwasubiri
kwa hamu, walipofika cha kwanza nilianza na John, “mzee baba, hebu njoo nje
tuyajenge” nilimwelekezea nje sababu alikuja na rafiki yake mwingine ambaye
nisingependa asikilize maongezi yetu ya siri, tulipofika nje nikaanza
kufunguka, “sasa mzee nisianze kukupanga tutapoteza muda” nilitengeneza
attention kwanza kwa John kabla sijafunguka, “mzee unamfaham binti wa darasa
lenu anayefahamika kwa jina la Grace!?” Kabla sijaendelea kumuelezea John
alionekana kulivuta tabasamu na kushindwa kujizuia na kuanza kucheka, “hahaha,
mkuu umemjulia wapi huyo mtoto, namfaham nipo nae group moja darasani na sio
nje ya hapo” Sikutaka kupoteza muda, nilimuelezea John hisia zangu na yeye
kuniahidi kunisahidia kwa jitihada zote ili nimmiliki.
Siku iliyofuata nilikuwa na kipindi kimoja jioni
CHIMWAGA nililisubiri hilo somo kwa hamu nikiangalia masaa kama hayasogei, muda
ulipokaribia nikamtumia ujumbe John na kumkumbusha kuwa leo ndio siku ya
kunitambulisha na kufahamiana zaidi na Grace kwenye kipindi cha CHIMWAGA,
Nilivaa jeans nyeusi na juu flana niliyoazima kwa rafiki yangu Grayson ninayesoma
nae BASO - Bach of Arts in Socialogy. Hakika nilinoga, lakini haya yalikuwa ni
mashambulizi ya chini nilokuwa nayaanzisha. Nilimpigia John mapema na
kumsisitiza ajitahidi kuwa na Grace waongozane wote wakija kwenye kipindi
CHIMWAGA.
Niliwahi kwenda kwenye malango ya CHIMWAGA
nikiwasubiri, John hakufanya makosa, niliwaona kwa mbali wakiwa wanakuja
walikuwa watatu na mmoja kati yao ilikuwa ni sura ngeni nisiitambue, nilizima
mziki wa simu yangu lakini sikuzivua earphone ili lisionekane dhumuni langu la kuwahi CHIMWAGA siku ya leo, wakiwa
wamekaribia nilionekana ni mtu mwenye hali ya ubize nisiwaone, “Justine!”
niligundua ni sauti ya John ikiniita kwa nyuma, nikiwa nageuka. “Waaoh, John
unafahamiana na Justine!?” ilisikika sauti ya Grace ambaye aliuliza swali
ambalo hakuwa katika muonekano wa kusubiri jibu, “Aaah, huyu ni pacha wangu,
roomate na nilisoma nae tangu secondary Morogoro, labda swali hilo nikuulize
wewe” John alijitetea. Nikawakatisha mazungumzo yao na kubadilisha mada,
“Nawaona mpo moto, Grace rafiki yako huyo pembeni anaitwa nani!?”. Kwa kuwa
niligundua Grace ni mpole, niliuliza swali kwa kujiamini. “Anna sogea
nikutambulishe” alimeza mate, Anna alivyotusogelea akaendelea, “huyu ni ndugu
yangu, wote tumetoka Dar, tukakutana huku”. Nikadakia “nafurahi kumfahamu” ili
asiendelee kueleza mengi kuhusu Anna ikiwa mlengwa wa movie ni yeye.
John alinifurahisha kwa kujiongeza, alimshika mkono
Anna na kuelekea nae chemba na kuniacha na Grace, kwa kweli nina asili ya uoga
lakini hofu iliniisha pale nilipogundua kuwa Grace ni muoga zaidi yangu, hivyo
nilijiamini. “Vipi maisha ya chuo!?” nilimuuliza, “Yako powa japo ni kazi sana
kukubaliana na haya mazingira, vipi na wewe!? Alijibu na kunigeuzia swali.
“Kwangu pia ni magumu, lakini ni huu ugeni ndio unatufanya tuwe wanyonge”
alidakia “Yes, ni kweli” nilistushwa na vibration ya simu yangu ilivyokuwa
inaita mfukoni, nilihisi John alikuwa ananipigia ameshaanza usumbufu,
kutahamaki hakuwa yeye bali ni roomate wangu mwingine, nikamuomba Grace
samahani kabla sijapokea simu, “bila samahani, endelea” Nilivyopokea kwa
kufupisha mazungumzo niliuliza “bro shida nini!?” akajibu “kijana pole kwa
usumbufu ila mwenzio nimeshikwa kinoma na kifua huku uliponiacha” Nikakumbuka
James alinitaarifu muda kuwa anatatizo la pumu na huwa inambana sana kipindi
hiki cha baridi, kwa kuwa room kwetu wote ni mwaka wa kwanza tulihitajika
CHIMWAGA hivyo hapakuwa na mtu ambaye anaweza kumpa msahada wa halaka kwa
kipindi hicho. Lecturer wetu pia alionekana kwa mbali anakuja kwa kujivuta,
nilikata simu na kumwambia Grace mazingira yaliyotokea yamenirazimu nirudi
hostel muda huu, nikampa simu yangu kwa kuashiria naomba namba zake za simu, alivyomaliza
kuzi’type nikapanda bodaboda, “niagie kwa John” hiyo ndiyo kauli ya mwisho
nilomwambia wakati bodaboda imeanza kwenda.
Njiani nilisononeka sana lakini nilikuwa sina budi
kuondoka kwa kuwa ni dharula ya ghafla, nilivyofika nikamkuta James yupo room
akiwa anapumua kwa shida huku mapigo ya moyo yakiwa yanadunda kwa kasi. “Sasa
bro haina kulemba, jiandae nikupeleke hospitali ukachomwe sindano ya kutuliza
maumivu” akajibu “nipo tayari, ni kuvaa sendo tu” nikamshika mkono na kuanza
kuelekea kwenye bajaji tayari kwenda hospitali, tukiwa ndani ya usafiiri
niliona ujumbe unaingia kwenye simu yangu, kuangalia lilikuwa ni jina la Grace,
ukisema “mgonjwa anaendeleaje?” Nilijifariji kimoyomoyo baada ya kukumbuka kuwa
mimi ndio niliyechukua namba zake, na zangu hakuziomba wala sikumtumia message
yoyote, hivyo bila shaka zangu atakuwa kachukua kwa John, nikamjibu “hali si
shwari, jamaa amebanwa na kifua ndio tumekaribia hospitali” akajibu “poleni,
utanijuza kinachoendelea” nikajibu “usijali, tuendelee kumuombea” baada ya
masaa mawili hali ya mgonjwa ilikuwa nafuu, tuliruhusiwa kurudi hosteli,
ilikuwa yapata saa 1:22 jioni, tukarudi room na kumpumzisha mgonjwa.
Nilimuacha akipumzika na nikaenda cafteria kuchukua
chakula, nikiwa nimebeba kontena kwenye folen ya msosi kuna mtu aliniziba macho
kwa nyuma, Lol! mguso wake haukuwa mgeni, kwa mikono laini kiasi kile, nilijua
bila shaka atakuwa ni Grace tu. “Aaaah, G! Unataka kufanya nini!?” nilitaka
kupaniki lakini alivyotoa mikono, hasira zote mwanaume zikaniisha, ilikuwa ni
uso kwa uso, aibu ikanishika mbele ya ule umati kwa kuwa sijazoea mambo ya kuch
kuch otaeh, “samahani kama nimekukwaza” alijistukia, “bila samahani” nikalivuta
tabasamu la uongo asigundue kitu, “eeeh niambie, mgonjwa anaendeleaje!?”
nikajibu “yupo powa, ndio ninamchukulia chakula” zamu yangu ya kuchukua msoso
ilifika hivyo nikapakuliwa na kumuacha Grace akiwa na Anna kwa nyuma, basi
nikawa nawasikilizia nao wapakuliwe tuondoke, “Justine usitusubiri, mimi
nikimaliza kula nitakuja kumuona mgonjwa, akikisha anakula chakula hi…cho.”
kabla hajamaliza kauli nilidakia “usiwaze” niliondoka nikiwa na furaha kwa kuwa
nia yangu ilikuwa inakwenda kufanikiwa.
Nilipeleka chakula haraka, nikafanya usafi chumba
chote, nikawapasha James na roomate mwingine kuwa mida ikifika nitawaweka nje
kwa muda hivyo ni vyema waniache na
mgonjwa nikiuguza ili mgeni akija tusiwe zaidi ya watatu, ombi langu lilipita
kwa kuwa ilikuwa ni taarifa na wala sio mjadala, hakika nilipania. Saa 2:15
iliingia message kuwa “ndio ninatoka, nitajie block number na room number”
nilijibu “karibu, block 03, number 335” ndipo nikaanza kuwatawanya roomate
wangu wengine na kuwatelekeza kwenye room nyingine za jirani, halikuwa jambo
geni kwa kuwa ni kawaida ya wanafunzi kufanya hivyo haswa kwenye mabweni ya
wanaume, hazikupita hata dakika kumi nilisikia “hoooodi” nilikohoa kikohozi cha
uongo kabla ya kuinuka na kwenda kufungua mlango, “karibu G!, ingia, tafadhali
usivue viatu, ni pachafu” alitoa mguno wa unafki “mmmmh, haya bhana. Eeeh James
yuko wapi!?” bila kufikiria mara mbili nilijibu “kuna kazi wamepewa class, yupo
group discussion” nikasikia mguno wa pili, awamu hii ulikuwa ni mrefu zaidi,
“mmmmmmmmmmh!” ndipo fahamu zikanijia kuwa Grace na James wapo darasa moja na
group moja, hivyo ukiwa muongo unatakiwa kuwa na kumbukumbu, kabla sijaanza
kutunga uongo mwingine wa kujitetea “karibu mgeni” sauti ya John ilisikika,
“Aaaah, ahsante nimekaribia.
Mazungumzo yalikuwa mengi, ilienda hadi saa tatu
usiku, kwa kuwa mgonjwa alikunywa maji mengi, kuna muda alitupisha kwenda
chooni ili akatoe haja ndogo, alivyotoka tu ndio nami nikaanza kutetemeka, ila
nilijipa moyo na kujikaza kishujaa, dakika chache ujumbe uliingia kwa simu
yangu, “haya nimekuachia show, ushidwe mwenyewe, nipo na James chumba cha pili”
ilikuwa ni message ya John iliyoniongezea joto kubwa na kuzidi kutetemeka,
“mbona message uliyoisoma imekupa kigugumizi, au ni tigopesa muamara umesoma!?”
lilikuwa ni swali la Grace, “aaah wapi, ni CR wetu ametupa taarifa ya kesho hakutokuwa
na kipindi asubuh “teh teh teh, usiniambie umenidanganya tena!?” round hii
Grace alishanikariri uongo wangu, nilisisitiza “ni kweli” nikameza mate kidogo
“Amini hivyo, ukijua ukweli utakusumbua” niliinama chini, nilivyoinuka macho
yetu yaligongana, mapigo ya moyo yalikuwa kasi lakini nae alionekana na
kushikwa na mshangao asiweze kuzungumza chochote, hakika alitambua kabisa nini
nilikuwa namaanisha, zilipita sekunde 20 tukiangaliana nisizungumze chochote,
kweli mimi ni domo zege, nilitamani kunyanyuka na kiss zito nimuoneshe kuwa nipo
vizuri lakini nilijiwazia moyoni kuwa movie za kizungu zisiniponze. “Justine!,
niliitwa kwa sauti ya mahaba, “naam”, niliulizwa “mgonjwa muda wote huo, au
kadondoka chooni!?” Aliuliza kwa tabasamu mithili ya mtu anayejua ninini
kinachoendelea, “Grace, hebu kuwa serious, sijui pa kuanzia ila kwa kufupisha
story kwa kweli NAKUPENDA, nisameh kwa kuwa imekuwa mapema ila nimeshindwa
kujizuia” sentence yangu ya mwisho ilinitoa hadi jasho, nilihisi kuutua mzigo
nilioubeba mwaka mzima, basi hali ya room ilibadilika, nilitamani kubadilisha
kauli nisiweze, neno lilishanitoka, “Justine, mmh please naomba uniruhusu
niondoke, leo nimekuja kumuona mgonjwa” aliongea kwa jazba. “Najua mama, naomba
unipe dakika kadhaa, utanielewa!” ghafla mood ikabadilika “please, next time!”
nikajikuta nipo kwenye movie za kikolea niinuke nimtulize kwa kiss lakini
nilijisumbua “naomba siku nyingine usiniite room kwenu, hata kwa habari ya
discusion” hio kauli ilitosha nijue amekasirika, akautoa mkono wangu uliokuwa
umekaribia kugusa mashavu yake na kufungua mlango kwa nguvu kwa lengo la
kusepa.
Mwili mzima ulijaa ganzi, nilijiona nina papara sana,
sikupaswa kukurupuka, kwani ni mapema mno, basi nilijipa moyo kuwa zile ni
hasira tu kesho mambo yatakuwa sawa, mawazo yangu yalikuwa na ukweli sababu
ilivyofika saa 5 usiku nikiwa natafakari, nilitakiwa usiku mwema,
nilipohadithia roommate wangu juu ya hiyo habari, niliambulia matani na majungu
kuwa nina haraka, nilitakiwa kusoma mazingira, hivyo natakiwa niwe mpole
kwanza, basi usiku nilikesha nikitafakari juu ya siku ya kesho nitaenda kwa
njia gani, nilitamani huu usiku ungekuwa wa baraka kwangu lakini ndege
amefyatua mtego sina budi kuanza upya, nilipotezea kutosoma ujumbe wake wa
message ilipofika asubuh nikampigia kumtakia asubuh njema lakini ilishindikana,
simu yake haikupokelewa, nikajipa tena moyo labda nimcheki baadae, moyo
uliniuma sana baada ya kuangalia ratiba ya madarasani na kugundua leo hatuna
kipindi CHIMWAGA, wazo likanijia la kumtafuta Anna, rafiki wa karibu na Grace
ili anisaidie kuweka mambo sawa, niliomba number zake kwa James nikapewa, mida
ya mchana nilichat nae na kumuomba kabla ya lunch nimuone, achague room au
cafteria. Alinipa uhuru wa kusema sehemu mimi, hivyo nilimuomba aje room
kwangu, saa 8 kasorobo alivyotoka kula alipitiliza Block 03 ninapoishi,
nilianza kumpeleleza kama ameshapewa habari ya taarifa iliyotokea jana,
alikataa katakata kuwa hakuna analojua, wakati huo tukiwa peke yetu room,
tukiwa tunashauriana juu ya hatua za kufanya za kumuweka Grace sawa, niliona macho
ya Anna yanaanza kubadilika, japo nilikuwa mshamba kwenye mambo ya mapenzi
lakini niligundua kuwa mwenzangu alikuwa kwenye ulimwengu mwingine, “Justine,
naamini ni ngumu kunielewa, hata ningekuwa wewe ingekuwa si rahisi kuamini
hili” aliamua kunifungukia “Mimi pia ni binadamu, naomba niziweke wazi hisia
zangu kwako, naomba nifichie aibu yangu, nakupenda” Akili ilizidi
kuchanganyikiwa lakini niliamini hizi ni njia za Grace kunijaribu “Nooo,
hauwezi kuwa serious” Anna alianza kutokwa na machozi mazito kuashiria kuwa
yupo makini na anachozungumza, “mbona unanichanganyia madawa Anna, ulisubiri
hadi nikwambie shida zangu ndio utake kuniharibia au!?”
niliongea kwa sauti ya juu hadi nikajistukia. “Okay, naomba ninyamaze na
uniruhusu niondoke kwako, na siwezi kukusaidia juu ya Grace, nakupenda”
aliufungua mlango wangu kwa nguvu na kutokomea, nilishanunua chakula cha mchana
kwa ajili ya kula lunch room lakini hakikuwa na radha tena, nilihisi kufanyiwa
mchezo, tena wa kaole kabisaa, haiwezekani mambo yote yanikute mimi ndani ya
siku mbili, wenzangu waliingia room na kunikuta kama nimechanganyikiwa,
niliwaomba kwanza nikajimwagie maji nitarudi kuwahadithia, nilipotoka bafuni
nilivyoanza kuwasimulia juu ya huo mkasa, James alithibitisha ni kweli kuwa
Anna alikuwa ananielewa tangu siku ya kwanza tuonane CHIMWAGA, na aliwahi
kumtumia yeye ili aje aniambie mimi lakini yeye hakunifikishia ujumbe sababu
aliwahi kumtongoza Anna na jitihada zake ziligonga mwamba…..
·
Kwa nini Justine apachukie CHIMWAGA.
·
Atachukua uamuzi gani baada ya kutongozwa na Anna.
·
Ni nini kitaendelea baada ya kutokea kwa hali hiyo ya
sintofahamu.
USIKOSE
SEHEMU YA PILI NA YA MWISHO YA SIMULIZI HII


Sehemu ya pili....
ReplyDeleteNice
ReplyDeleteVerynice
ReplyDeleteVerynice
ReplyDelete