NAKUCHUKIA CHIMWAGA - SEHEMU YA KWANZA



NAKUCHUKIA CHIMWAGA
Ukiachana na siafu, sisimizi ndio wadudu wadogo ambao hukusanyika kwa pamoja kuongozana kwenye shughuli zao za kila siku, mfano kwenye mambo ya ujenzi na hata kupeana sapoti kwenye maswala ya mnuso, hakika huu msululu umeshona, kushoto na kulia ni kundi kubwa la wanafunzi wakielekea CHIMWAGA zikisikika sauti tofauti za wanachuo wa course mbalimbali kwa kuwa somo la leo wanasoma wanafunzi wa faculty zote kwa mwaka wa kwanza wa masomo.
Nilistushwa na mkono mlaini ulonigusa begani ukanifanya nipunguze speed ya hatua zangu na kuvua earphone, “Msimbe!!!, kukuita kote huko hujanisikia!?” nikiwa namalizia kutoa earphone ya sikio la pili akaongezea “mwanzoni nilijua nakufananisha, za masiku!?” nikamjibu “safi tu” japo kuwa sura yake bado ilikuwa ngeni machoni pangu. “Sorry, nikumbushe walau jina kama hautojali” akatahamaki “hakika nimekufananisha, duniani wawili wawili kwa kuwa Msimbe sio wa kunisahau mimi”
Nikiwa bado nimemkazia macho, niligundua hakika alikuwa ni binti mrembo mwenye kila sifa za uzuri ambao si rahisi kukutana na aina ya watu hao mara kwa mara, nilianza kujiona mwenye bahati kusimama na msichana mwenye sifa za kipekee mbele ya umati wa wanachuo, nilitamani kuwa Msimbe kweli, ili niendelee kuongozana na binti huyo ambaye alionekana kuishiwa nguvu ya maongezi baada ya kunifananisha.
“Pole, naitwa Justine. Ni mwaka wa kwanza, natokea mkoa wa Morogoro, ni kweli utakuwa umenifananisha, kwani una uhusiano gani na Msimbe! Mmepotezana muda sana!?” nilimuacha ajielezee, tukiwa bado tunaongozana “Ahsante, alikuwa rafiki yangu nilisoma nae shule ya msingi miaka saba iliyopita” alijibu huku akipepesa macho chini, mfano wa mwizi aliyeshikwa na ushahidi wa mali ya dhuluma mkononi mwake.
“Usijali, naweza kulijua jina lako tafadhali!?”, “naitwa Grace pia ni mwaka wa kwanza” nilitamani kubadilisha mada ili tuendeleze conversation lakini tulikuwa tayari tumeingia malango ya Chimwaga, na kwa uchache wa haya maongezi tuliyoongea hayakutosha kuwa na ujasiri wa kuchukua hata namba zake za simu. Aligeuka nyuma na kuungana na jopo la marafiki zake na kuniaga, “sawa Justine, wacha niwasubiri wenzangu niingie nao” nami bila hiana “Usijali Grace, mimi natangulia ndani, ulisema unachukua course gani?” nilimuuliza kwa kupata urahisi wa kumtafuta siku nyingine. “BADS” alifupisha akimaanisha Bach of Arts in Development Study, tukaachana.
Niliingia darasani nikiwa bado natafakari uumbaji wa Mungu, nilijinong’oneza mwenyewe kwa kujiambia ‘Mungu ni fundi’ nikiwa darasani sikuelewa somo lolote kutoka kwa Lecture mawazo yote niliyaelekeza kwa Grace, nilitamani kipindi kiishe mapema nimtafute John ambaye ni roomate wangu ambaye pia anachukua BADS ili nimuelezee juu ya habari ya siku nzima ya leo iliyozidi kunichanganya, upole na ukauzu wangu nikiwa chuo ulinifanye niwe mnyonge kila utakaponiona sababu kwangu ilikuwa ni kazi kuchangamana na marafiki wapya, huwa inachukua muda mrefu sana kuwazoea, pindi lilivyoisha kama kawaida nilivaa earphone zangu na kurejea hostel.
Licha ya kuweka sauti ya juu ya muziki kwenye simu, sikusikiliza neno lolote lililotajwa kwenye nyimbo, nikiendelea kupepesa macho kwa kudhani nitaonana tena na yule binti mrembo lakini kwa wingi wa watu waliotoka CHIMWAGA haikuwa rahisi kumtambua, niliongeza hatua kukazana kurudi hostel nimuwahi John. Nilipofika room sikukutana na roomate yoyote niliwasubiri kwa hamu, walipofika cha kwanza nilianza na John, “mzee baba, hebu njoo nje tuyajenge” nilimwelekezea nje sababu alikuja na rafiki yake mwingine ambaye nisingependa asikilize maongezi yetu ya siri, tulipofika nje nikaanza kufunguka, “sasa mzee nisianze kukupanga tutapoteza muda” nilitengeneza attention kwanza kwa John kabla sijafunguka, “mzee unamfaham binti wa darasa lenu anayefahamika kwa jina la Grace!?” Kabla sijaendelea kumuelezea John alionekana kulivuta tabasamu na kushindwa kujizuia na kuanza kucheka, “hahaha, mkuu umemjulia wapi huyo mtoto, namfaham nipo nae group moja darasani na sio nje ya hapo” Sikutaka kupoteza muda, nilimuelezea John hisia zangu na yeye kuniahidi kunisahidia kwa jitihada zote ili nimmiliki.
Siku iliyofuata nilikuwa na kipindi kimoja jioni CHIMWAGA nililisubiri hilo somo kwa hamu nikiangalia masaa kama hayasogei, muda ulipokaribia nikamtumia ujumbe John na kumkumbusha kuwa leo ndio siku ya kunitambulisha na kufahamiana zaidi na Grace kwenye kipindi cha CHIMWAGA, Nilivaa jeans nyeusi na juu flana niliyoazima kwa rafiki yangu Grayson ninayesoma nae BASO - Bach of Arts in Socialogy. Hakika nilinoga, lakini haya yalikuwa ni mashambulizi ya chini nilokuwa nayaanzisha. Nilimpigia John mapema na kumsisitiza ajitahidi kuwa na Grace waongozane wote wakija kwenye kipindi CHIMWAGA.
Niliwahi kwenda kwenye malango ya CHIMWAGA nikiwasubiri, John hakufanya makosa, niliwaona kwa mbali wakiwa wanakuja walikuwa watatu na mmoja kati yao ilikuwa ni sura ngeni nisiitambue, nilizima mziki wa simu yangu lakini sikuzivua earphone ili lisionekane dhumuni  langu la kuwahi CHIMWAGA siku ya leo, wakiwa wamekaribia nilionekana ni mtu mwenye hali ya ubize nisiwaone, “Justine!” niligundua ni sauti ya John ikiniita kwa nyuma, nikiwa nageuka. “Waaoh, John unafahamiana na Justine!?” ilisikika sauti ya Grace ambaye aliuliza swali ambalo hakuwa katika muonekano wa kusubiri jibu, “Aaah, huyu ni pacha wangu, roomate na nilisoma nae tangu secondary Morogoro, labda swali hilo nikuulize wewe” John alijitetea. Nikawakatisha mazungumzo yao na kubadilisha mada, “Nawaona mpo moto, Grace rafiki yako huyo pembeni anaitwa nani!?”. Kwa kuwa niligundua Grace ni mpole, niliuliza swali kwa kujiamini. “Anna sogea nikutambulishe” alimeza mate, Anna alivyotusogelea akaendelea, “huyu ni ndugu yangu, wote tumetoka Dar, tukakutana huku”. Nikadakia “nafurahi kumfahamu” ili asiendelee kueleza mengi kuhusu Anna ikiwa mlengwa wa movie ni yeye.
John alinifurahisha kwa kujiongeza, alimshika mkono Anna na kuelekea nae chemba na kuniacha na Grace, kwa kweli nina asili ya uoga lakini hofu iliniisha pale nilipogundua kuwa Grace ni muoga zaidi yangu, hivyo nilijiamini. “Vipi maisha ya chuo!?” nilimuuliza, “Yako powa japo ni kazi sana kukubaliana na haya mazingira, vipi na wewe!? Alijibu na kunigeuzia swali. “Kwangu pia ni magumu, lakini ni huu ugeni ndio unatufanya tuwe wanyonge” alidakia “Yes, ni kweli” nilistushwa na vibration ya simu yangu ilivyokuwa inaita mfukoni, nilihisi John alikuwa ananipigia ameshaanza usumbufu, kutahamaki hakuwa yeye bali ni roomate wangu mwingine, nikamuomba Grace samahani kabla sijapokea simu, “bila samahani, endelea” Nilivyopokea kwa kufupisha mazungumzo niliuliza “bro shida nini!?” akajibu “kijana pole kwa usumbufu ila mwenzio nimeshikwa kinoma na kifua huku uliponiacha” Nikakumbuka James alinitaarifu muda kuwa anatatizo la pumu na huwa inambana sana kipindi hiki cha baridi, kwa kuwa room kwetu wote ni mwaka wa kwanza tulihitajika CHIMWAGA hivyo hapakuwa na mtu ambaye anaweza kumpa msahada wa halaka kwa kipindi hicho. Lecturer wetu pia alionekana kwa mbali anakuja kwa kujivuta, nilikata simu na kumwambia Grace mazingira yaliyotokea yamenirazimu nirudi hostel muda huu, nikampa simu yangu kwa kuashiria naomba namba zake za simu, alivyomaliza kuzi’type nikapanda bodaboda, “niagie kwa John” hiyo ndiyo kauli ya mwisho nilomwambia wakati bodaboda imeanza kwenda.
Njiani nilisononeka sana lakini nilikuwa sina budi kuondoka kwa kuwa ni dharula ya ghafla, nilivyofika nikamkuta James yupo room akiwa anapumua kwa shida huku mapigo ya moyo yakiwa yanadunda kwa kasi. “Sasa bro haina kulemba, jiandae nikupeleke hospitali ukachomwe sindano ya kutuliza maumivu” akajibu “nipo tayari, ni kuvaa sendo tu” nikamshika mkono na kuanza kuelekea kwenye bajaji tayari kwenda hospitali, tukiwa ndani ya usafiiri niliona ujumbe unaingia kwenye simu yangu, kuangalia lilikuwa ni jina la Grace, ukisema “mgonjwa anaendeleaje?” Nilijifariji kimoyomoyo baada ya kukumbuka kuwa mimi ndio niliyechukua namba zake, na zangu hakuziomba wala sikumtumia message yoyote, hivyo bila shaka zangu atakuwa kachukua kwa John, nikamjibu “hali si shwari, jamaa amebanwa na kifua ndio tumekaribia hospitali” akajibu “poleni, utanijuza kinachoendelea” nikajibu “usijali, tuendelee kumuombea” baada ya masaa mawili hali ya mgonjwa ilikuwa nafuu, tuliruhusiwa kurudi hosteli, ilikuwa yapata saa 1:22 jioni, tukarudi room na kumpumzisha mgonjwa.
Nilimuacha akipumzika na nikaenda cafteria kuchukua chakula, nikiwa nimebeba kontena kwenye folen ya msosi kuna mtu aliniziba macho kwa nyuma, Lol! mguso wake haukuwa mgeni, kwa mikono laini kiasi kile, nilijua bila shaka atakuwa ni Grace tu. “Aaaah, G! Unataka kufanya nini!?” nilitaka kupaniki lakini alivyotoa mikono, hasira zote mwanaume zikaniisha, ilikuwa ni uso kwa uso, aibu ikanishika mbele ya ule umati kwa kuwa sijazoea mambo ya kuch kuch otaeh, “samahani kama nimekukwaza” alijistukia, “bila samahani” nikalivuta tabasamu la uongo asigundue kitu, “eeeh niambie, mgonjwa anaendeleaje!?” nikajibu “yupo powa, ndio ninamchukulia chakula” zamu yangu ya kuchukua msoso ilifika hivyo nikapakuliwa na kumuacha Grace akiwa na Anna kwa nyuma, basi nikawa nawasikilizia nao wapakuliwe tuondoke, “Justine usitusubiri, mimi nikimaliza kula nitakuja kumuona mgonjwa, akikisha anakula chakula hi…cho.” kabla hajamaliza kauli nilidakia “usiwaze” niliondoka nikiwa na furaha kwa kuwa nia yangu ilikuwa inakwenda kufanikiwa.
Nilipeleka chakula haraka, nikafanya usafi chumba chote, nikawapasha James na roomate mwingine kuwa mida ikifika nitawaweka nje kwa muda  hivyo ni vyema waniache na mgonjwa nikiuguza ili mgeni akija tusiwe zaidi ya watatu, ombi langu lilipita kwa kuwa ilikuwa ni taarifa na wala sio mjadala, hakika nilipania. Saa 2:15 iliingia message kuwa “ndio ninatoka, nitajie block number na room number” nilijibu “karibu, block 03, number 335” ndipo nikaanza kuwatawanya roomate wangu wengine na kuwatelekeza kwenye room nyingine za jirani, halikuwa jambo geni kwa kuwa ni kawaida ya wanafunzi kufanya hivyo haswa kwenye mabweni ya wanaume, hazikupita hata dakika kumi nilisikia “hoooodi” nilikohoa kikohozi cha uongo kabla ya kuinuka na kwenda kufungua mlango, “karibu G!, ingia, tafadhali usivue viatu, ni pachafu” alitoa mguno wa unafki “mmmmh, haya bhana. Eeeh James yuko wapi!?” bila kufikiria mara mbili nilijibu “kuna kazi wamepewa class, yupo group discussion” nikasikia mguno wa pili, awamu hii ulikuwa ni mrefu zaidi, “mmmmmmmmmmh!” ndipo fahamu zikanijia kuwa Grace na James wapo darasa moja na group moja, hivyo ukiwa muongo unatakiwa kuwa na kumbukumbu, kabla sijaanza kutunga uongo mwingine wa kujitetea “karibu mgeni” sauti ya John ilisikika, “Aaaah, ahsante nimekaribia.
Mazungumzo yalikuwa mengi, ilienda hadi saa tatu usiku, kwa kuwa mgonjwa alikunywa maji mengi, kuna muda alitupisha kwenda chooni ili akatoe haja ndogo, alivyotoka tu ndio nami nikaanza kutetemeka, ila nilijipa moyo na kujikaza kishujaa, dakika chache ujumbe uliingia kwa simu yangu, “haya nimekuachia show, ushidwe mwenyewe, nipo na James chumba cha pili” ilikuwa ni message ya John iliyoniongezea joto kubwa na kuzidi kutetemeka, “mbona message uliyoisoma imekupa kigugumizi, au ni tigopesa muamara umesoma!?” lilikuwa ni swali la Grace, “aaah wapi, ni CR wetu ametupa taarifa ya kesho hakutokuwa na kipindi asubuh “teh teh teh, usiniambie umenidanganya tena!?” round hii Grace alishanikariri uongo wangu, nilisisitiza “ni kweli” nikameza mate kidogo “Amini hivyo, ukijua ukweli utakusumbua” niliinama chini, nilivyoinuka macho yetu yaligongana, mapigo ya moyo yalikuwa kasi lakini nae alionekana na kushikwa na mshangao asiweze kuzungumza chochote, hakika alitambua kabisa nini nilikuwa namaanisha, zilipita sekunde 20 tukiangaliana nisizungumze chochote, kweli mimi ni domo zege, nilitamani kunyanyuka na kiss zito nimuoneshe kuwa nipo vizuri lakini nilijiwazia moyoni kuwa movie za kizungu zisiniponze. “Justine!, niliitwa kwa sauti ya mahaba, “naam”, niliulizwa “mgonjwa muda wote huo, au kadondoka chooni!?” Aliuliza kwa tabasamu mithili ya mtu anayejua ninini kinachoendelea, “Grace, hebu kuwa serious, sijui pa kuanzia ila kwa kufupisha story kwa kweli NAKUPENDA, nisameh kwa kuwa imekuwa mapema ila nimeshindwa kujizuia” sentence yangu ya mwisho ilinitoa hadi jasho, nilihisi kuutua mzigo nilioubeba mwaka mzima, basi hali ya room ilibadilika, nilitamani kubadilisha kauli nisiweze, neno lilishanitoka, “Justine, mmh please naomba uniruhusu niondoke, leo nimekuja kumuona mgonjwa” aliongea kwa jazba. “Najua mama, naomba unipe dakika kadhaa, utanielewa!” ghafla mood ikabadilika “please, next time!” nikajikuta nipo kwenye movie za kikolea niinuke nimtulize kwa kiss lakini nilijisumbua “naomba siku nyingine usiniite room kwenu, hata kwa habari ya discusion” hio kauli ilitosha nijue amekasirika, akautoa mkono wangu uliokuwa umekaribia kugusa mashavu yake na kufungua mlango kwa nguvu kwa lengo la kusepa.
Mwili mzima ulijaa ganzi, nilijiona nina papara sana, sikupaswa kukurupuka, kwani ni mapema mno, basi nilijipa moyo kuwa zile ni hasira tu kesho mambo yatakuwa sawa, mawazo yangu yalikuwa na ukweli sababu ilivyofika saa 5 usiku nikiwa natafakari, nilitakiwa usiku mwema, nilipohadithia roommate wangu juu ya hiyo habari, niliambulia matani na majungu kuwa nina haraka, nilitakiwa kusoma mazingira, hivyo natakiwa niwe mpole kwanza, basi usiku nilikesha nikitafakari juu ya siku ya kesho nitaenda kwa njia gani, nilitamani huu usiku ungekuwa wa baraka kwangu lakini ndege amefyatua mtego sina budi kuanza upya, nilipotezea kutosoma ujumbe wake wa message ilipofika asubuh nikampigia kumtakia asubuh njema lakini ilishindikana, simu yake haikupokelewa, nikajipa tena moyo labda nimcheki baadae, moyo uliniuma sana baada ya kuangalia ratiba ya madarasani na kugundua leo hatuna kipindi CHIMWAGA, wazo likanijia la kumtafuta Anna, rafiki wa karibu na Grace ili anisaidie kuweka mambo sawa, niliomba number zake kwa James nikapewa, mida ya mchana nilichat nae na kumuomba kabla ya lunch nimuone, achague room au cafteria. Alinipa uhuru wa kusema sehemu mimi, hivyo nilimuomba aje room kwangu, saa 8 kasorobo alivyotoka kula alipitiliza Block 03 ninapoishi, nilianza kumpeleleza kama ameshapewa habari ya taarifa iliyotokea jana, alikataa katakata kuwa hakuna analojua, wakati huo tukiwa peke yetu room, tukiwa tunashauriana juu ya hatua za kufanya za kumuweka Grace sawa, niliona macho ya Anna yanaanza kubadilika, japo nilikuwa mshamba kwenye mambo ya mapenzi lakini niligundua kuwa mwenzangu alikuwa kwenye ulimwengu mwingine, “Justine, naamini ni ngumu kunielewa, hata ningekuwa wewe ingekuwa si rahisi kuamini hili” aliamua kunifungukia “Mimi pia ni binadamu, naomba niziweke wazi hisia zangu kwako, naomba nifichie aibu yangu, nakupenda” Akili ilizidi kuchanganyikiwa lakini niliamini hizi ni njia za Grace kunijaribu “Nooo, hauwezi kuwa serious” Anna alianza kutokwa na machozi mazito kuashiria kuwa yupo makini na anachozungumza, “mbona unanichanganyia madawa Anna, ulisubiri hadi nikwambie shida zangu ndio utake kuniharibia au!?” niliongea kwa sauti ya juu hadi nikajistukia. “Okay, naomba ninyamaze na uniruhusu niondoke kwako, na siwezi kukusaidia juu ya Grace, nakupenda” aliufungua mlango wangu kwa nguvu na kutokomea, nilishanunua chakula cha mchana kwa ajili ya kula lunch room lakini hakikuwa na radha tena, nilihisi kufanyiwa mchezo, tena wa kaole kabisaa, haiwezekani mambo yote yanikute mimi ndani ya siku mbili, wenzangu waliingia room na kunikuta kama nimechanganyikiwa, niliwaomba kwanza nikajimwagie maji nitarudi kuwahadithia, nilipotoka bafuni nilivyoanza kuwasimulia juu ya huo mkasa, James alithibitisha ni kweli kuwa Anna alikuwa ananielewa tangu siku ya kwanza tuonane CHIMWAGA, na aliwahi kumtumia yeye ili aje aniambie mimi lakini yeye hakunifikishia ujumbe sababu aliwahi kumtongoza Anna na jitihada zake ziligonga mwamba…..

·         Kwa nini Justine apachukie CHIMWAGA.
·         Atachukua uamuzi gani baada ya kutongozwa na Anna.
·         Ni nini kitaendelea baada ya kutokea kwa hali hiyo ya sintofahamu.
USIKOSE SEHEMU YA PILI NA YA MWISHO YA SIMULIZI HII

Comments

Post a Comment

Popular Posts